Fransisko Choe Kyonghwan

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Fransisko Choe Kyonghwan (Taraekkol, 1804 - Seoul, 12 Septemba 1839) alikuwa katekista wa Korea ambaye, kisha kupelekwa mbele ya liwali kwa imani ya Kikristo, hakukubali kuikana. Akiwa mfungwa gerezani na kuteswa kwa namna mbalimbali hakuacha kamwe sala na kazi ya katekesi hadi alipofikia kifodini[1].

Ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya dini yao katika miaka 17911888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.

Yeye[2] na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[3]

Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe ni tarehe ya kifodini chake[4].

Remove ads

Mazingira

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[5] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[6].

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads