Fransisko wa Fabriano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Fransisko Venimbeni wa Fabriano (2 Septemba 1251 - 22 Aprili 1322) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo kutoka Fabriano (Marche, Italia).

Mapema alianza kuheshimiwa kama mwenye heri. Hatimaye Papa Pius VI alithibitisha uhalali wa heshima hiyo tarehe 1 Aprili 1775.
Remove ads
Maisha
Kisha kumaliza masomo yake ya sayansi za jamii na falsafa, alijiunga na Wafransisko mwaka 1267, akajikita katika masomo ya teolojia, uandishi na utume katika mji wake asili na maeneo ya kandokando.
Alikuwa wa kwanza kuipatia konventi ya shirika lake maktaba kubwa.
Maandishi
Maandishi yake ("Chronica Marchiæ et Fabriani", "De veritate et excellentiâ Indulgentiæ S. Mariæ de Portiuncula", "Opusculum de serie et gestis Ministrorum Generalium", "Ars Prædicantium", mbali na "Hotuba" na vitabu vingine) yamepotea karibu yote.
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads