Fuzuli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fuzuli
Remove ads

Fuzuli (Kar./Kituruki فضولی) ilikuwa jina la kisanii la mshairi Muhammad bin Suleyman oğlu Füzuli (Kar. محمد بن سليمان) (takriban 1495 1556). Alikuwa mshairi mashuhuri wa Milki ya Osmani aliyeandika kwa lugha za Kituruki, Kiajemi na Kiarabu. Kituruki chake kilikuwa cha Kiazeri. Alikuwa pia mtaalamu wa hisabati na na falaki.

Kwa eneo la utawala nchini Azerbaijan, angalia Fizuli.
Thumb
Fuzûlî (1483?–1556)

Fuzuli alizaliwa mnamo 1483 au 1495 katika eneo la Iraq ya leo ama mjini Najaf au Karbala. Familia yake ilitoka katika kabila ya Waturuki wahamiaji waliowahi kukaa mjini kwa vizazi kadhaa. Alipata elimu nzuri. Hakuna habari zaidi zenye uhakika juu ya maisha yake isipokuwa alikufa kutokana na ugonjwa wa kuambukizwa.

Mashairi yake yamehifadhiwa yakihesabiwa kati ya mifano bora ya mashairi ya Kituruki wa wakati wake. Aliandika mengi juu ya mapenzi lakini pia beti za kupinga makosa ya umma kwa mfano ufisafi:

سلام وردم رشوت دگلدر ديو آلمادىلر
Selâm verdim rüşvet değildir deyü almadılar.[1]
Nilisema "salaam" lakini hawakukubali kwa sababu haikuwa hongo.


Thumb
Ukurasa kutoka mashairi yake Fuzuli


Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads