Georgi Zhukov

From Wikipedia, the free encyclopedia

Georgi Zhukov
Remove ads

Georgi Konstantinovich Zhukov (1 Desemba 1896 - 18 Juni 1974) alikuwa jenerali wa Umoja wa Kisovyeti. Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia aliongoza Jeshi Jekundu hadi ushindi wake juu ya Ujerumani ya Adolf Hitler. Baada ya vita aliendelea kuwa Waziri wa Ulinzi na mwanachama wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti.

Thumb
Zhukov mnamo mwaka 1944
Thumb
Zhukov katika Berlin baada ya ushindi, pamoja na jenerali Mwingereza Montgomery
Remove ads

Maisha

Zhukov alizaliwa katika familia ya wakulima maskini[1] kwenye Kaluga Oblast ya Urusi ya Magharibi wakati wa utawala wa kifalme. Alipokuwa kijana alipaswa kuingia katika jeshi la Urusi. Wakati wa kuporomoka kwa jeshi hilo katika mapinduzi ya Kirusi alijiunga na Jeshi Jekundu[2] alipoendeelea kupanda ngazi.

Baada ya kipindi cha mtakaso wa kisiasa chini ya Josef Stalin maafisa wengi wa jeshi waliuawa au kufukuzwa, Zhukov aliweza kuingia haraka katika ngazi ya juu.

Alitumwa Mongolia alipoongoza Jeshi Jekundu dhidi ya uvamizi wa Japani na kushinda maadui[3].

Baada ya uvamizi wa Ujerumani katika Umoja wa Kisovyeti, aliongoza utetezi wa Leningrad, Moscow, na Stalingrad[4] . Kwenye mwisho wa vita aliongoza vikosi vilivyoteka Berlin alipopokea majenerali Wajerumani waliosalimisha amri mnamo 9 Mei 1945.

Baada ya vita alikuwa gavana wa kijeshi katika Ujerumani ya Mashariki kwa muda mfupi halafu alishushwa cheo na Stalin aliyeogopa umaarufu wake[5]. Mwaka 1953 alirudi Moscow wakati wa kifo cha Stalin na uongozi mpya ulimpa uwaziri wa ulinzi[6]; alipokelewa pia katika kamati kuu ya chama.

Mnamo 1957 alishtakiwa kuwa na uhusiano wa karibu mno na jenerali Eisenhower wa Marekani alipaswa kustaafu.

Mnamo 1958 alianza kutunga wasifu zake lakini chama cha kikomunisti iliingila kwa kudai mabadiliko. Sehemu za wasifu zilitolewa miaka mingi baada ya kido chake na baada ya mwisho wa Ukomunisti nchini Urusi.

Mwaka 1968 alipigwa mara ya kwanza na upoozaji akaaga dunia baada kupooza mara ya pili mwaka 1974.

Zhukov alipokea heshima nyingi kwa mafanikio yake ya kijeshi akikumbukwa kama shujaa wa kitaifa.

Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads