Gideoni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Gideoni (kwa Kiebrania גדעון - Ghide'on) alikuwa mwana wa Yoas, wa kabila la Manase.

Thumb
Gideoni alivyochorwa na Maarten van Heemskerck (1550 hivi).

Mungu alimuita awe mwamuzi wa Israeli kwa miaka 40; kisha kupewa ishara ya umande kwenye ngozi iliyotandazwa ardhini, kwa nguvu ya Mungu alibomoa altare ya Baal akakomboa sehemu kubwa ya nchi kutoka mikono ya Wamidiani kama kitabu cha Waamuzi (6-8) kinavyosimulia[1].

Kwa jinsi anavyosifiwa na Waraka kwa Waebrania, anaheshimiwa katika imani ya Wakristo wote ulimwenguni kama mtakatifu kulingana na ushuhuda wake katika kipindi chake cha kuwa mwamuzi wa Israeli.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Septemba[2].

Remove ads

Maisha yake

Alipoitwa na Mungu alijitetea kwa kusisitiza udogo na ufukara wake, lakini akajaliwa ishara zote alizoziomba ili kuhakikishiwa msaada (Amu 6:11-24,36-40).

Sura ya 7 inasimulia Mungu alivyopunguza askari wake ili ionekane wazi kuwa ushindi ni wa Mungu mwenyewe, hautegemei uhodari na wingi wa watu au silaha zao. Ni kawaida ya kazi ya Mungu kuonyesha uweza wake katika udhaifu wa binadamu.

Waisraeli walipotaka Gideoni awe mfalme wao, akakataa katakata ili Bwana tu aendelee kuwatawala (Amu 8:22-23), lakini wazo hilo likaendelea kuenea, ingawa wengine walilipinga (Amu 9:1-21).

Remove ads

Sala yake (Amu 6:15)

"Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu".

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads