Gobani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Gobani (alifariki Ufaransa, 670) alikuwa mmonaki padri wa Ukristo wa Kiselti kutoka Ireland.
Kama alivyothibitisha Beda Mheshimiwa[1], alikuwa mwanafunzi wa Fursei abati, aliyefanya kazi kubwa kueneza imani na umonaki kotekote katika visiwa vya Britania, hasa kati ya Waanglia[2][3].
Huyo alipohamia Ufaransa, Gobani alimfuata; hatimaye akawa mkaapweke kwenye msitu wa Voas, karibu na kijiji chenye jina lake, Saint-Gobain, Aisne.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, pengine mfiadini.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads