Goodluck Jonathan

From Wikipedia, the free encyclopedia

Goodluck Jonathan
Remove ads

Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan (alizaliwa 20 Novemba 1957)[1] alikuwa rais wa Nigeria tangu Januari 2010. Awali hakuchaguliwa lakini alikabidhiwa madaraka akiwa makamu wa rais mgonjwa Umaru Yar'Adua aliyemtangulia na baada ya kifo chake aliapishwa kama rais. Katika uchaguzi wa kitaifa wa Aprili 2011 alirudishwa madarakani.

Ukweli wa haraka Makamu wa Rais, mtangulizi ...
Remove ads

Elimu na maisha ya awali

Jonathan alizaliwa katika familia ya Wakristo wa kabila ya Ijaw kwenye delta ya mto Niger.[2] Alisoma shule za msingi Otuoke na Oloibiri na tangu 1971 shule ya sekondari ya Mater Dei mjini Imiringi. 1975 hadi 1977 alifanya kazi ya idara ya ushuru na kodi. 1977 akajiandikisha kama mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Port Harcourt katika idara ya zoolojia. Baada ya kumaliza kwa digrii ya bachela alifanya kazi ya ualimu wa shule mjini Iresi. Aliendelea kusoma Chuo Kikuu hadi kupata digrii za MSc na daktari ya falsafa katika zoolojia. 1993 alikuwa makamu wa mkurugenzi wa kamati ya maendeleo ya maeneo ya kutoa mafuta Nigeria akiwajibika kwa mambo ya kuhifadhi mazingira. 1998 aliingia katika siasa.[3]

Jonathan amemwoa Patience Faka Jonathan akiwa na watoto 2 [4]

Remove ads

Maisha ya kisiasa

Gavana wa jimbo la Bayelsa

Jonathan alijiunga na chama cha People's Democratic Party (PDP) mwaka 1998.[2] 1999 aliteuliwa kuwa makamu wa gavana. Gavana Diepreye Alamieyeseigha aliondolewa madarakani mwaka 2005 kutokana na mashtaka ya rushwa Jonathan alimfuata akawa gavana wa Bayelsa.

Mwaka 2006 mke wa Jonathan alishtakiwa na Halmashauri ya kupambana na rushwa kwa makosa ya kuficha pesa zisizo halali. [5]

Makamu wa rais

Mwezi wa Desemba 2006 mgombea wa urais Umaru Yar'Adua alimchagua Jonathan kama makamu wake kabla ya uchaguzi wa kitaifa wa 2007. [6] Kabla ya kura Jonathan alishambuliwa na wanamgambo tarehe 20 Aprili 2007 waliojaribu kumwua bila kufanikiwa. [7]

Baada ya ushindi wa Yar'Adua Jonathan alikuwa makamu wa rais kuanzia tarehe 29 Mei 2007.

Urais

Raisi Yar'Adua aligonjeka 2009 akaondoka nchini kwenda Saudia kwa matibabu. Baada ya rais Yar'dua kukaa miezi mfululizo katika hospitali nchini Saudia mahakama kuu ilimpa madaraka ya rais. Yar'Adua alipoaga dunia tarehe 5 Mei 2010 Jonathan aliapishwa siku iliyofuata kuwa rais wa 14 wa Nigeria.

Alimteua aliyewahi kuwa gavana wa jimbo la Kaduna kuwa makamu wake. [8][9]

Jonatahan aligombea urais katika uchaguzi wa 16 Aprili 2011 aliposhinda katika awamu ya kwanza kwa kupata kura 22,495,187 na angalau robo ya kura zote katika theluthi mbili za majimbo ya Nigeria. Mpinzani wake mkuu Buhari wa CPC alipewa kura 12,214,853 pekee. Watazamaji wa kimataifa walitangaza uchaguzi kuwa huru na kweli.[10]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads