Guido van Rossum

From Wikipedia, the free encyclopedia

Guido van Rossum
Remove ads

Guido van Rossum, (alizaliwa 31 Januari, 1956) ni mtayarishajiwa programu (programa) nchini Uholanzi anayejulikana zaidi kama mwanzilishi wa lugha ya programu ya Python, ambaye alikuwa na wadhifa wa benevolent dictator for life (BDFL) hadi alipojiuzulu kutoka wadhifa huo mnamo Julai 2018.[1][2] Alibaki kuwa mshiriki wa Baraza la Uendeshaji la Python hadi mwaka 2019, na akajiondoa kwenye uteuzi wa uchaguzi wa mwaka 2020.[3]

Thumb
Van Rossum akiwa kwenye mkutano wa O'Reilly Open Source (OSCON) mwaka 2006
Remove ads

Maisha na Elimu

Van Rossum alizaliwa na kukulia nchini Uholanzi, ambapo alipata shahada ya uzamili katika hisabati na sayansi ya kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam mnamo 1982. Ana kaka yake, Just van Rossum, ambaye ni mbunifu wa aina (type designer) na mpanga programu ambaye alibuni chapa iliyotumiwa kwenye nembo ya Python.[4]

Van Rossum anaishi Belmont, California, na mkewe Kim Knapp,[5] na mtoto wao wa kiume.[6][7][8] Kulingana na ukurasa wake wa nyumbani na mikusanyiko ya majina ya Kiholanzi, " van " katika jina lake lina herufi kubwa anapotajwa kwa jina la ukoo pekee, lakini sio wakati wa kutumia jina lake la kwanza na la mwisho kwa pamoja.[9]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads