Haumea

From Wikipedia, the free encyclopedia

Haumea
Remove ads

Haumea (alama: 🝻)[1] ni sayari kibete inayozunguka jua letu katika umbali mkubwa kwenye ukanda wa Kuiper. Ilitambuliwa mwaka 2004. Ina umbo la duaradufu; kipenyo chake baina ya ncha zake ni kilomita 1,138 lakini kipenyo kwenye ikweta ni kati ya km 2322 na km 1704. Umbo hili linatokana na mzunguko wa haraka kwenye mhimili wake.

Thumb
Haumea na miezi yake
Thumb
Mbingirio wa Haumea

Haumea ina miezi miwili: Hiiaka na Namaka.

Haumea inapita Njia Mzingo yake ya kuzunguka Jua katika muda wa miaka 283 na miezi 6.[2]

Periheli yake ina umbali wa vizio astronomia 35, afeli wa vizio astronomia 51 kutoka Jua.

Obiti ina mwinamo wa nyuzi 28,2° dhidi ya ekliptiki.

Masi yake ni takriban theluthi moja ya Pluto. Umbo halifanani na tufe; umbo la Haumea limefananishwa na kiazi au sigara. Vipimo vyake vinakadiriwa kuwa kilomita 2,322 × 1,701 × 1,138.

Nadharia moja inajaribu kueleza umbo na mzunguko wake wa haraka kutokana na mgongano na gimba kubwa takriban miaka bilioni 4 iliyopita.[3]. Kutokana na mgongano huu inadhaniwa ya kwamba vipande vingi vya gimba la awali viliachana na Haumea vikiifuata sasa kama wingu la vipande vidogo.[4]

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads