Pluto
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kuhusu matumizi ya jina "Utaridi" kwa sayari hii tazama chini kwa "jina"

Remove ads
Pluto (alama: [1] au
[2]) ni sayari kibete inayozunguka jua ng'ambo ya obiti ya Neptuni.
Masi yake ni hasa mwamba na barafu. Kipenyo chake ni km 2,390.
Katika mwendo wake inakata njia ya Neptuni kwa sababu njia yake ina umbo la duaradufu kali.
Remove ads
Miezi
Pluto ina miezi mitano inayoitwa Charon, Styx, Nix, Kerberos na Hydra. Charon ni kama nusu ya ukubwa wa Pluto (kipenyo km 1200) na umbali wa wastani ni km 19,410. Styx, Nix, Kerberos na Hydra ni miezi midogo (vipenyo: km 10-25, 56x26, 31 na 43x33) yenye umbali wa km 42,600, 48,600, 57,700 na 64,700 kutoka Pluto.
Sayari au sayari kibete?
Pluto ilikuwa ikitambulika kama sayari ya tisa katika mfumo wa Jua toka mwaka 1930 hadi Agosti 2006. Vipimo vipya vilileta wasiwasi juu ya swali: Je, sayari ni kitu gani?, hasa baada ya kugundua magimba ya ziada nje ya Pluto yanayokaribia ukubwa wake lakini hayafai kuitwa sayari.
Umoja wa kimataifa wa wanaastronomia uliondoa Pluto katika orodha ya sayari kwenye mkutano wake wa mwaka wa 2006. Badala yake wameiita sayari kibete. Hata hivyo baadhi ya wanaastronomia walipinga uamuzi huu.
Remove ads
Jina
Jina "Pluto" linamtaja mungu mtawala wa kuzimu katika mitholojia ya Roma ya Kale. Limechaguliwa kwa sayari hii kutokana na umbali wake na jua na giza kubwa liliko sawa na hali ya giza ambayo ni mfano wa kuzimu.
Vitabu kadhaa vinatumia jina la Kiswahili Utaridi[3] [4] [5] kwa kufuata kamusi ya KAST; lakini mabaharia Waswahili wametumia jina hili la "Utaridi" tangu miaka mingi kwa ajili ya sayari ya kwanza (ing. "Mercury").[6]
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads