Hedmark

From Wikipedia, the free encyclopedia

Hedmarkmap
Remove ads

Hedmark ilikuwa moja kati ya majimbo ya Norwei, likipakana na Sør-Trøndelag, Oppland na Akershus.

Thumb
Mahali pa jimbo la Hedmark nchini Norwei.
Thumb
Atnsjøen na Rondane mwezi June 2009

Ngazi ya utawala ya jimbo hili ilikuwa mjini Hamar.

Hedmark ilikuwa upande wa kaskazini-mashariki mwa sehemu ya Østlandet, sehemu ya kusini ya jimbo. Ilijumuisha sehemu ndefu ya mipaka ya Uswidi, Jimbo la Dalarna na Jimbo la Värmland. Maziwa makubwa jimboni humo ni Femunden na Mjøsa. Pia ilijumuisha sehemu za Glomma.

Kijiografia, Hedmark iliwahi kugawanyika katika maeneo yafuatayo: Hedemarken, mashariki mwa Mjøsa, Østerdalen, kaskazini mwa Elverum, na Glåmdalen, kusini mwa Elverum. Hedmark na Oppland yalikuwa majimbo pekee nchini Norwei ambayo hayana ukanda wa pwani. Hedmark pia ilishawahi kuandaa baadhi ya mashindano ya 1994 Winter Olympic Games.

Jimboni humo miji mashuhuri ilikuwa pamoja na Hamar, Kongsvinger, Elverum na Tynset. Hedmark ni moja kati maeneo ambayo hayakujengwa sana nchini Norwei, jinsi ilivyo nusu ya wakazi wake wanaishi katika maeneo ya vijijini. Uwingi wa watu hutazamwa sana kule katika maeneo ya matajiri ambapo ni Mjøsa na pande zingine za kusini-mashariki. Misitu mikubwa ya jimboni hapa ilisambaza mbao vya kutosha nchini Norwei; vigogo vilikuwa vikisafirishwa kupitia Glomma kwa njia ya bahari lakini siku hizi vinasafirishwa kwa njia ya lori au treni.

Kwa sasa imeunganishwa na Oppland kuunda jimbo jipya la Innlandet.

Remove ads

Manispaa jimboni

Thumb
Manispaa za Hedmark
Maelezo zaidi Ukubwa, Jina ...
Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads