Helena Mtakatifu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Helena (kwa Kigiriki: Ἑλένη, Helénē; kwa Kilatini: Flavia Iulia Helena Augusta; 246/248 – Roma, 330 hivi) alikuwa mke wa kaisari Constantius Chlorus.

Alijitokeza kwa bidii zake za kusaidia fukara; pia alikuwa anaingia makanisani kwa moyo wa ibada akijichanganya na umati wa waumini [1].
Alipohiji Yerusalemu ili kuheshimu mahali pa kuzaliwa, kuteseka na kufufuka Yesu Kristo, alitembelea pango na msalaba wake akapajengea mabasilika ya fahari [2].
Ni maarufu hasa kama mama wa Konstantino Mkuu aliyemuelekeza kupenda Ukristo na hivyo alichangia uanzishaji wa uhuru wa dini katika Dola la Roma baada ya miaka 250 ya dhuluma dhidi yake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads