Kindi-jua

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kindi-jua
Remove ads

Kindi-jua ni wanyama wadogo wa jenasi Heliosciurus katika kabila Protoxerini la familia Sciuridae. Mkia yao una miviringo myeusi na kahawia au kijivu. Kama kindi wote spishi hizi hupitisha takribani saa zote mitini na huteremka kwa nadra ardhini. Hupatikana mara nyingi wakipumzika juani, sababu ya jina lao. Wanatokea misitu ya Afrika ya Magharibi, ya Kati na ya Mashariki kutoka Senegali mpaka Eritrea na Zimbabwe. Hula mbegu, makokwa, matunda, matumba, machipukizi, wadudu, mayai na mijusi, ndege na wanyama wadogo.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi

Remove ads

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads