Herode Agripa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
'Herode Agripa, kwa Kigiriki 'Ἡρώδης Ἀγρίππας, Herodes Agrippas, (10 KK – 44 BK), alikuwa mfalme wa sehemu kubwa ya Palestina katika karne ya 1 kutoka ukoo wa Herode Mkuu, babu yake .

Baba yake alikuwa Aristobulo IV na mama yake Berenike.[1]
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Marcus Julius Agrippa, ambalo alipewa kwa heshima ya mwanasiasa wa Roma Marcus Vipsanius Agrippa.
Alianza kutawala mwaka 41 BK.
Ndiye anayesemwa katika Matendo ya Mitume (Agano Jipya, Biblia ya Kikristo), hasa kama muuaji wa Yakobo Mkubwa muda mfupi kabla hajafa mwenyewe.
Kumbe mwandishi wa Kiyahudi Yosefu Flavio anamsifu na kumuita "Agripa Mkuu".[2]
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads