Hidulfi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Hidulfi (pia: Hidulf, Hildulf, Hidulfus, Hidulphus, Hiduiphus, Hidulphe, Hydulphe; alifariki 707) alikuwa mmonaki halafu askofu wa 29 wa Trier, leo nchini Ujerumani, kwa miaka mitano. Baadaye aling'atuka na kwenda kuishi upwekeni kwenye milima ya Vosges, leo nchini Ufaransa, ila alifuatwa na wengi akawaanzishia monasteri ya Moyenmoutier akaiongoza hadi kifo chake [1][2].

Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Julai[3][4].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads