Inna Modja

Mwanamuziki From Wikipedia, the free encyclopedia

Inna Modja

Inna Bocoum (kwa jina lingine Inna Modja; alizaliwa Bamako, Mali, Mei 19, 1984, ni mwanamuziki na mwanamitindo kutoka Mali. "Modja" humaanisha "mbaya, sio nzuri" katika lugha ya Kifulde.[1][2]

Thumb
Picha ya Inna Modja

Utoto na ujana

Alizaliwa katika familia ya kifula, mtoto wa sita kati ya watoto saba, Inna Bocoum alipata jina lake la kisanii kutoka kwa mama yake, ambaye alimpachika jina la utani "Inna Modja", ambalo maana yake ni "Inna ni mtu mbaya" au "Inna sio mtu mzuri" katika lugha ya kifulfulde. Alipofikisha umri wa miaka sita, wazazi wake walimuunganisha na kwaya. Nyumbani, baba yake alimuhimiza ajiendeleze kwa kumchezea nyimbo kadhaa alizokuwa akizipenda (za wasanii kama Ray Charles, Ella Fitzgerald, Otis Redding na Sarah Vaughan). Pia alishawishiwa na ndugu zake waliomzidi umri, walioendelea zaidi katika muziki wa Thrash Punk, miaka ya '80/'90 Rap, Heavy Metal, Blues, Soul na Disco.

Inna hupinga na kusema ukeketaji wa wanawake FGM, yeye mwenyewe na dada zake ni wahanga wa ukeketaji, walikeketwa bila idhini ya wazazi wao, tukio ambalo ameliimba kwenye moja ya nyimbo zake. Amekwishafanyiwa upasuaji wa kurekebisha maumbile yake. Pia hukemea ukatili dhidi ya wanawake, ambao ameuonesha kwenye video ya wimbo wake uitwao "La Valse de Marylore".

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.