Issyk Kul

From Wikipedia, the free encyclopedia

Issyk Kulmap
Remove ads

Issyk Kul (kwa Kikirgizi: Yssykköl "ziwa moto"; kwa Kirusi: Иссык-Куль) ni ziwa kubwa zaidi la nchi ya Kirgizia katika Asia ya Kati.

Ukweli wa haraka Ziwa Issyk Kul ...

Ziwa hilo liko katika milima ya Tian Shan na uso wake upo mita 1,607 juu ya usawa wa bahari. Eneo la maji ni km2 6236 na hivyo ni ziwa la mlimani kubwa la pili duniani baada ya Ziwa Titicaca (Amerika Kusini). Mito 118 inapeleka maji yao katika Issyk Kul. Muhimu zaidi ni mito ya Jergalan, Tjup, Dschuku, Karakol na Jeti-Ogus.

Remove ads

Tabia za pekee

Maji ya Yssyk Kul hayagandi wakati wa baridi ingawa halijoto ya hewa hupoa hadi sentigredi 20 chini ya sifuri. Inaaminiwa sababu yake hasa ni mwendo wa kuchanganya maji ya chini (yenye halijoto ya °C 4) na maji ya usoni (yanayopoa zaidi wakati wa baridi). Sababu ya ziada ni kiasi kidogo cha chumvi katika maji ya ziwa kinachofikia asilimia 0.6 (maji ya bahari huwa na % 3.5)

Ziwa hilo halina njia ya kutoka, kwa hiyo maji yote yanayoingia hulingana na kiasi kinachopotea tena kwa njia ya uvukizaji.

Riwaya kadhaa za mwandishi Genghis Aitmatov zinasimulia hadithi za Issyk Kul.

Remove ads

Matumizi

Zamani Issyk Kul ilikuwa na maana kwa uvuvi wa samaki; siku hizi hutumiwa zaidi kwa utalii. Karibu na ziwa iko miji ya Karakol na Cholpon-Ata.

Wakati wa Umoja wa Kisovyeti (hadi mwaka 1991) maeneo makubwa ya ziwa na mwambao yalikuwa maeneo ya kijeshi; wanamaji walifanya hapa utafiti na majaribio ya topido.

Picha

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads