Kifo cha Yesu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kifo cha Yesu
Remove ads
Remove ads

Kifo cha Yesu msalabani kilitokea huko Yerusalemu, nchini Israeli, siku ya Ijumaa, labda tarehe 7 Aprili 30 BK[1][2].

Thumb
Mchoro wa Diego Velázquez, Yesu msulubiwa, 1631, Prado (Madrid, Hispania) unaonyesha anwani juu ya kichwa chake.

Tukio hilo[3], pamoja na ufufuko wa Yesu unaosadikiwa na Ukristo kutokea siku ya tatu (Jumapili ya Pasaka), ndiyo kiini cha imani ya dini hiyo mpya iliyotokana na ile ya Uyahudi.

Kwa Wakristo fumbo hilo la Pasaka ndilo kilele cha historia ya wokovu inayotangazwa na Biblia ya Kikristo.

Fumbo hilo lilisababisha kazi nyingi za sanaa ya Kikristo, hasa uchoraji na uchongaji.

Remove ads

Historia

Injili zote nne zinasimulia tukio hilo kinaganaga kuliko mengine yote ya maisha ya Yesu Kristo: ni kama simulizi la saa baada ya saa[4].

Kadiri ya (Mk 14:43–15:45; Math 26:46–27:60; Lk 22:47–23:53; Yoh 18:3–19:42), Ponsyo Pilato, liwali wa Palestina (26-36), aliamua Yesu aadhibiwe hivyo kulingana na shtaka la viongozi wa Wayahudi waliodai kwamba mtuhumiwa alijitangaza kuwa mfalme na kupinga mamlaka ya Kaisari wa Roma, kwa wakati huo Tiberius, ingawa Pilato alikuwa ametambua shtaka halikuwa la kweli, bali lilitokana na husuda[5][6][7][8].

Kadiri ya Injili ya Yohane, Pilato mwenyewe alisisitiza kwamba, katika maandishi yaliyotakiwa kuwajulisha watu sababu ya adhabu hiyo, iwekwe wazi kwamba Yesu aliuawa kama mfalme wa Wayahudi, ingawa neno hilo lilichukiza viongozi wa taifa.

Maneno ya ilani hiyo yaliandikwa katika lugha tatu:

Yesu akiwa msalabani alisema maneno kadhaa. Kati ya hayo, ni maarufu maneno saba yaliyoripotiwa na Injili yakimuelekea Mungu Baba, Bikira Maria, Mtume Yohane na mhalifu aliyesulubiwa pamoja naye.

Remove ads

Maelezo ya teolojia

Kifo cha Yesu kinaelezwa na Injili na vitabu vingine vya Agano Jipya kuwa kafara kwa fidia ya dhambi za ulimwengu mzima.[9]

Yesu alipokufa, nafsi yake ya Kimungu iliendelea kushikamana na roho na mwili vilivyotengana: kwa hiyo mwili wake uliozikwa haukuweza kuoza kaburini; roho yake ilishukia kuzimu kuwatoa waadilifu waliomtangulia awaingize pamoja naye mbinguni. “Mwili wake aliuawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri” (1Pet 3:19). “Roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu” (Mdo 2:31).

Remove ads

Mitazamo tofauti

Tangu kale walitokea watu waliokanusha ukweli wa kifo cha Yesu, hasa waliosema yeye hakuwa na mwili halisi, bali alionekana tu kuwa nao.[10][11].

Waislamu wanashikilia msimamo huo, kwamba Yesu hajafa kwa namna yoyote[12], bali alipalizwa mbinguni.

Tanbihi

Loading content...

Marejeo

Loading content...

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads