Joseph John Thomson
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Joseph John Thomson (18 Desemba 1856 – 30 Agosti 1940) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa anajulikana kwa kugundua elektroni. Mwaka wa 1906 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Mwaka wa 1908 alipewa cheo cha Sir cha Uingereza.


Pamoja na gunduzi zake muhimu alikuwa pia mwalimu bora akachangia hivyo kwenye maendeleo ya sayansi. Mmoja wa wanafunzi wake alikuwa Ernest Rutherford aliyemfuata baadaye kuwa pfofesa wa fizikia kwenye Chuo Kikuu cha Cambridge. Nane kati ya wasaidizi wake waliendelea kupata baadaye pia tuzo za Nobel katika fani za fizikia au kemia (Francis William Aston, Charles Glover Barkla, Niels Bohr, Max Born, William Henry Bragg, Owen Willans Richardson, Ernest Rutherford, Charles Wilson). Mwanawe George Thomson alshinda mwaka 1937 tuzo ya Nobel kwa kuthebitisha tabia ya elektroni kuwa kama wimbi.
Hadi kifo alikuwa Mkristo wa Kanisa la Kianglikana.[1]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads