Jennifer Garner

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jennifer Garner
Remove ads

Jennifer Anne Affleck [1] (hasa hufahamika kwa jina lake la kuzaliwa kama Jennifer Garner; amezaliwa 17 Aprili 1972), ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Garner amejipatia umaarufu mkubwa kwa kucheza kwake kama kachero wa CIA, Sydney Bristow, katika kipindi cha mfululizo wa TV cha Alias, ambacho kilikuwa kikirushwa hewani na televisheni ya ABC kwa misimu mitano ambayo ilianza kuanzia 2001 hadi 2006. Wakati anafanyakazi kwenye Alias, amepata kucheza nyusika chache-chache kwenye mafilamu makubwa-makubwa kama vile Pearl Harbor (2001) na Catch Me if You Can (2002). Tangu hapo, Garner ameonekana kwenye nyusika kadha wa kadha akiwa kama mwigizaji mwandamizi vilevile mwigizaji mkuu kwenye mamiradi makubwa ikiwa ni pamoja na Daredevil (2003), 13 Going on 30 (2004) na Juno (2007). Ameolewa na mwigizaji na mwongozaji wa filamu Ben Affleck, ambaye kwa pamoja wameweza kujipatia watoto wawili wa kike.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Kazi yake ...
Remove ads

Maisha ya awali

Garner ni wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto watatu wa kike waliozaliwa huko mjini Houston, Texas. Mama yake, Patricia Ann, alikuwa mwalimu wa lugha ya Kiingereza kutoka mjini Oklahoma, na baba yake, Bill John Garner, alifanyakazi kama mhandisi wa kemikali katika Union Carbide. Wakati alivyokuwa na umri wa miaka minne, kazi ya baba yake na Union Carbide iliwahamisha kuelekea mjini Princeton, West Virginia, na kisha baadaye mjini Charleston, West Virginia, ambapo Garner aliweka makazi hadi alipofikisha kipindi chake cha miaka ya chuo.[2] Alimsifia dada yake mkubwa, Melissa Lynn Garner Wylie, ambaye anaishi mjini Boston, Massachusetts, kama chanzo cha mafanikio yake.[3] Mdogo wake wa kike ni Susannah Kay Garner Carpenter.[4]

Msimamo wa Garner kiukuaji ni pamoja na kwenda kanisani kila Jumapili, hapaki majipambo ya usoni wala vibikini, na kusubiri hadi angalau alivyofikisha miaka 16 aruhusiwe masikio yake kutobolewa, ambapo, baadaye alileta mzaha kidogo, kaifanya familia yake "kuwa mbali kidogo na Uamish."[5][6] Ameanza kuchukua masomo ya ballet akiwa na umri wa miaka mitatu hadi kipindi chake chote cha ujana, lakini hajajibidisha yeye mwenyewe ili kufikia kiwango cha ballerina wa kisasa.[7] Garner alisoma katika shule ya George Washington High School ya mjini Charleston, West Virginia. Mnamo mwaka wa 1990, alijiunga na Chuo Kikuu cha Denison kilichopo mjini Ohio, ambapo alijikita zaidi katika masuala ya uigizaji na kufanya kazi kadha wa kadha kuhusiana na masuala ya utayarishaji na tamthilia.[8] Baada ya kuhitimu chuoni Denison, ambapo alijiunga na umoja wa kina dada wa Pi Beta Phi, kunako mwaka wa 1994.[9]

Remove ads

Maisha binafsi

Mnamo 19 Oktoba 2000, Garner ameolewa na mwigizaji Scott Foley, ambaye alikutana naye kwenye seti ya tamthili ya Felicity kunako 1998. Baada ya kutengana na Foley mnamo mwezi wa Machi 2003, Garner amefungua faili la talaka kunako mwezi wa Mei 2003, na kutaja tofauti zao ambazo haziwezi kupatanishwa, na wawili hao wakatalikiana rasmi kunako tar. 30 Machi 2004.[10] Kufuatia kutengana kwake, Garner akaanza kutembea na mwigizaji-mshirika mwenzake kwenye Alias Michael Vartan kuanzia mwezi wa Agosti 2003 hadi Machi 2004.[11][12]

Wakati fulani katikati mwa 2004, Garner ameanza kutembea na mwigizaji-mshirika wa katika Daredevil Ben Affleck na wawili hao walionesha uhusiano wao mbele ya kadamnasi wakiwa kama wapenzi waliohudhuria katika siku ya ufunguzi wa Boston Red Sox-World Series kunako Oktoba 2004.[13] Tangu uhusiano wake na Affleck, kwanza akiwa kama demu wake na kisha baadaye kuwa mkewe.[14]

Remove ads

Filmografia

Filamu

Maelezo zaidi Mwaka, Jina ...

Television

Maelezo zaidi Miaka, Jina ...
Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads