Jerry Rawlings

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jerry Rawlings
Remove ads

Jerry Rawlings (Accra, koloni la Gold Coast, 22 Juni 1947 - 12 Novemba 2020) alikuwa rais Ghana na afisa wa zamani wa jeshi. Aliongoza nchi ya Ghana kutoka mwaka wa 1981 hadi mwaka wa 2001 na kwa muda mfupi mwaka wa 1979. Pamoja na viongozi wengine wa kijeshi, walitawala mpaka mwaka wa 1992. Baadaye, Rawlings aliunda National Democratic Congress (NDC) na aliwahi kuwa rais wa Ghana mara mbili.

Thumb
Maelezo zaidi Rais wa Ghana (1st President of the 4th Republic), Makamu wa Rais ...
Remove ads

Maisha ya utotoni

Wazazi wake waliitwa Victoria Agbotui na James Ramsey John. Mama alitokea Gold Coast. Baba aliishi katika ngome ya Douglas katika Kirkcudbrightshire, nchi ya Uskoti. Makabila ya mama yake yalikuwa Nzema na Ewe lakini hii haikuathiri siasa zake. 

Elimu na huduma kwa jeshi

Alienda shule ya upili ya Achimota kisha alisoma Chuo cha Achimota. Alijunga na Jeshi la Anga la Ghana muda mfupi baadaye. Katika Jeshi la Anga, aliishi Takoradi, katika Mkoa wa Magharibi wa Ghana, ili kuendelea na masomo. Yeye alihitimu mnamo mwezi wa kwanza mwaka 1969 na kuwa Afisa Mwanahewa. Yeye alikuwa luteni katika jeshi la anga la Ghana mwezi wa nne mwaka wa 1978.

Rawlings aliongoza vita mbili za mapinduzi katika mwaka wa 1979 dhidi ya Ignatius Kutu Acheampong na Jenerali Fred Akuffo na mwaka wa 1981 dhidi ya Rais Hilla Limann. Rawlings hakufurahishwa na serikali ya Ignatius Kutu Acheampong ambaye alipindua serikali nyingine na kuanza uongozi mwezi wa kwanza mwaka wa 1972. Rawlings hakumpenda Acheampong kwa sababu alishutumiwa kwa ufisadi na kuifanya nchi ya Ghana kutegemea mifumo ya serikali ya kabla ya ukoloni. Hii ilisababisha kuporomoka kwa uchumi na kuongezeka kwa viwango vya umaskini.

Tarehe 15 Mei 1979, wiki tano kabla ya uchaguzi wa kitaifa, Rawlings na askari wengine sita walifanya mapinduzi dhidi ya serikali ya Jenerali Acheampong, lakini walishindwa na alikamatwa na Jeshi la Ghana. Alihukumiwa hadharani kifo. Wakati wakingojea kuuawa kwake, Rawlings alitoroka kutoka kizuizini tarehe 4 mwezi wa sita mwaka wa 1979 na kikundi cha askari. Mnamo mwaka wa 1982 alijaribu mapinduzi mengine dhidi ya Rais Hilla Limann na akafanikiwa. Rawlings alitawala kupitia Provisional National Defence Council (PNDC) hadi mwaka wa 1992. Kisha akawania urais na akashinda.

Remove ads

Familia

Yeye alifunga ndoa na Nana Konadu Agyeman. Walikutana katika chuo Kikuu cha Achimota. Wameza watoto wanne; watatu wa kike wanaoitwa Ezanetor Rawlings, Yaa Asantewaa, na Amina Rawlings, pia mmoja wa kiume anayeitwa Kimith Rawlings.

Maisha ya baada ya urais

Mnamo mwezi Novemba mwaka wa 2000, Rawlings alipewa tuzo ya kwanza ya Year of Volunteers 2001 Eminent Person na katibu wa Umoja wa Mataifa. Baada ya kupokea tuzo, alizungumza kuhusu kujitolea. Mnamo mwezi Oktoba mwaka wa 2010, yeye alikuwa mwakilishi wa Jumuiya ya Afrika nchini Somalia. Baadaye alokuwa anatoa hotuba katika vyuo vikuu.

Viungo vya nje

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads