Accra

mji mkuu wa Ghana From Wikipedia, the free encyclopedia

Accra
Remove ads

Accra ni mji mkuu wa Ghana ukiwa na wakazi 1 650 000[1]. Accra ni kitovu cha uchumi, biashara na mawasiliano ya nchi. Iko ndani ya mkoa wa Accra Kuu.

Thumb
Mji mkuu wa Ghana, Accra
Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...
Thumb
Mahali pa Accra katika Ghana
Thumb
Labadi Beach
Thumb
Accra mjini
Remove ads

Historia

Accra ilianzishwa na Waga katika karne ya 15 BK kama kituo cha biashara na Wareno. Wareno walijenga boma kwa ajili ya biashara hiyo na Waswidi, Waholanzi, Wafaransa, Waingereza na Wadenmark walifuata.

Eneo la Accra ya leo liliendelea kuwa mji kati ya boma tatu za Uingereza (Jamestown), Denmark (Osu) na Uholanzi (Ussherstown). Maeneo hayo matatu leo ni kitovu cha mji wa kisasa.

Baada ya Waingereza kushinda Waashanti, Accra ikawa mji mkuu wa koloni la Pwani la dhahabu. Mji uliendelea kukua baada ya kujengwa kwa reli na bandari.

Katika miaka ya 1940 Accra ilikuwa pia mwanzo wa upinzani dhidi ya Waingereza ulioleta uhuru wa Ghana mwaka 1956.

Leo hii Accra imepata mji pacha wa karibu wa Tema baada ya kuhamishwa kwa viwanda na bandari kwenda Tema inayounganishwa na Accra yenyewe kwa reli na barabara kuu.

Remove ads

Marejeo

Loading content...

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads