Jimbojina

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Jimbojina (kwa Kilatini: "diocesis titularis") ni dayosisi ya zamani ya Kanisa Katoliki ambayo kwa sasa imefutwa isiwe na eneo wala watu, lakini kumbukumbu yake inatunzwa hai kwa kuichagulia askofu asiye mkuu wa jimbo lolote[1]. Huyo haishi huko wala hana mamlaka yoyote juu ya eneo la zamani la jimbo hilo[2].

Makala hii kuhusu "Jimbojina" inatumia neno au maneno ambayo si ya kawaida; matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Utaratibu huo ulianza mwaka 1514. Mara chache unafuatwa na Waorthodoksi pia[3].

Annuario Pontificio inatoa orodha ya majimbojina yote ya Kanisa Katoliki[4].

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads