Jura

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jura
Remove ads

Kipindi cha Jura (jurassic) ni kipindi cha pili cha kijiolojia katika enzi ya kimesozo. Ilianza miaka milioni 200 iliyopita, na ilimalizika miaka milioni 145 iliyopita. Kipindi cha Kijura kilitokea baada ya kipindi cha Trias (triassic) na Chaki.

Thumb
Dinosauri wakionyeshwa kati ya miti ya kisasa
Remove ads

Jina

Jina linatokana na milima ya Jura (Uswisi) ambako mara ya kwanza matabaka ya miamba ya mashapo yaligunduliwa kama dalili za kipindi maalumu katika historia ya Dunia. Kwa Kiingereza umbo la "Jurassic" ni kawaida.

Tabianchi ya Jura

Wakati wa Jura, tabianchi ya Dunia ilikuwa na joto na mvua nyingi kuliko leo. Viwango vya dioksidi kabonia hewani na usawa wa bahari pia vilikuwa juu kuliko leo.

Mwanzoni mwa kipindi cha Jura mabara ya Dunia yalikuwa pamoja yakiunda bara kuu la Pangaia lililoanza kuvunjika wakati ule. Juu kabisa ilikuwa inaanza kuvunjika na kuunda chanzo cha Bahari Atlantiki, na kusababisha Bahari nyembamba ya Atlantiki.

Remove ads

Gandunia

Mwanzoni mwa kipindi cha Jura, bara kuu la Pangaia liligawanyika kwa vipande vya Laurasia upande wa kaskazini na Gondwana upande wa kusini. Mchakato huu uliounda hatimaye mabara ya leo ulichukua muda mrefu sana.

Kwenye mwisho wa Jura, Amerika Kusini ilikuwa imeanza kuachana na Afrika. Upande wa magharibi wa Amerika Kaskazini, safu za milima zilianza kutokea zilizoendelea kuwa Milima ya Rocy Mountains. [1]

Uhai - wanayama

Uhai duniani uliendelea kufuata mabadiliko yaliyowahi kuanza wakati wa Trias. Jura ilikuwa kipindi cha kwanza cha kustawi kwa dinosauri. Nyayo zao zilipatikana mahali mbalimbali ndani ya miamba ya wakati ule.

Mifupa ya ndege asilia ya archaeopteryx ilipatikana pia katika miamba ya Jura, pamoja na visukuku vya kwanza vya mamalia vinavyopatikana pia ndani ya miamba ya Jura. [2] Mamalia hao walikuwa wadogo tu.

Remove ads

Uhai - mimea

Kutoka kipindi hicho kuna visukuku vingi vya miti iliyofanana na misonobari. Mimea ya kangaga ilipatikana kwa wingi pia, spishi kadhaa zilikuwa kubwa kama miti. [3]

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads