Justin Long

From Wikipedia, the free encyclopedia

Justin Long
Remove ads

Justin Jacob Long (amezaliwa tar. 2 Juni 1978) ni mwigizaji wa filamu na vipindi vya televisheni kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa nyusika zake za kwenye filamu za Hollywood kama vile Galaxy Quest, Jeepers Creepers, Dodgeball, Waiting..., Accepted, Live Free or Die Hard, He's Just Not That into You, Drag Me to Hell, na Youth in Revolt, Alpha and Omega, na tashihisi yake ya Mac kwenye kampeni za matangazo ya Apple ya "Get a Mac".

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Kazi yake ...
Remove ads

Maisha ya awali

Long alizaliwa mjini Fairfield, Connecticut. Baba yake, R. James Long, alikuwa mwanafalsafa na profesa wa Kilatini katika Chuo Kikuu cha Fairfield, na mama yake, Wendy Lesniak,[2] mwigizaji ambaye ameigiza zaidi kwenye majukaa. Long amekulia katika makuzi ya Romani Katoliki.[3] Bibi yake ni Msicili.[4] Kaka yake mkubwa, Damian, ni mwigizaji mtaani vile vile mwalimu na mwongozaji wa tamthilia kwenye shule ya Weston High School. Ndugu yake mdogo, Christian, ameonekana kwenye filamu ya ndugu yake Accepted kama mleta bahati wa shule. Long amehitimu kwenye shule ya Fairfield College Preparatory School, shule ya Jumuiya ya Yesu, na Vassar College, ambapo alikuwa mchekeshaji kwenye moja ya kundi lililoitwa Laughingstock na kushiriki kwenye michezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Butterflies Are Free. Ameacha chuo mapema ili ajiendeleze zaidi na shughuli za uigizaji. Kabla ya kuacha, Long alifanyakazi katika chuo Kikuu cha Sacred Heart mjini Fairfield, Connecticut, akiwa kama mwelekezi/mashauri ya kikundi cha watoto.

Remove ads

Filmografia

Maelezo zaidi Mwaka, Filamu ...
Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads