Justiniani I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Justiniani I
Remove ads

Justiniani I au Justiniani Mkuu (jina kamili kwa Kilatini: Flavius Petrus Sabbatius Iustinianus Augustus; kwa Kigiriki Φλάβιος Πέτρος Σαββάτιος Ἰουστινιανός, Flávios Pétros Sabbátios Ioustinianós; Tauresium, Dardania,[1] leo nchini Masedonia Kaskazini[2] takriban 482 - Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 14 Novemba, 565) alikuwa kaisari wa Dola la Bizanti kuanzia mwaka wa 527 hadi kifo chake.

Thumb
Justiniani I anavyoonekana katika mozaiki ya wakati wake katika Basilika la San Vitale, Ravenna, Italia.

Justiniani alijitahidi kurudisha Dola la Roma katika fahari yake ya zamani (renovatio imperii, yaani kufanya upya dola) na kwa ajili hiyo alipigania upande wa magharibi dhidi ya wavamizi. Hata hivyo alifaulu kiasi tu.[3]

Mke wake na malkia wa Bizanti aliitwa Theodora; aliaga dunia mwaka wa 548. Hawakuwa na watoto walioishi. Hivyo Justiniani I alifuatwa kama kaisari na mpwa wake Justin II.

Huheshimiwa na Wakristo Waorthodoksi na Walutheri kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Novemba au 27 Novemba[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads