Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ni muungano wa Walutheri katika nchi ya Tanzania.

Ukweli wa haraka Mkuu wa kanisa:, Uhusiano: ...

Mwaka 1938 makanisa saba ya Kilutheri yaliungana kama Muungano wa Makanisa ya Kilutheri, na tarehe 19 Juni 1963 yakawa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.[1]

Lengo la KKKT ni kuwapa watu nafasi ya kumfahamu Yesu Kristo ili kupata uzima wa milele. Kanisa limejengwa juu ya msingi wa Yesu Kristo, linaongozwa na Neno la Mungu kama linavyopatikana katika Agano la Kale na Agano Jipya (Biblia ya Kikristo), na limeimarishwa katika sakramenti.

KKKT linaongozwa na Mkuu wa kanisa (Askofu Mkuu[2]) na maaskofu ishirini na sita kutoka dayosisi ishirini na saba, wakiwa na wanachama zaidi ya milioni 8 hivi [3] wanaolifanya kuwa la pili duniani kati ya makanisa ya Kilutheri (baada ya lile la Uswidi).

Ofisi kuu ya KKKT iko katika mji wa Arusha.

KKKT lina uhusiano na All Africa Conference of Churches (AACC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Lutheran World Federation (LWF) na Lutheran Mission Cooperation (LMC).

KKKT ni chama kinachowapa wanachama chake nafasi ya kumwabudu Mungu, kupata elimu ya Kikristo na huduma nyingi nyingine.

Remove ads

Matawi

  • Elimu (Sekondari na Chuo Kikuu)
  • Fedha na Utawala
  • Afya na Utabibu (Hospitali 21 na zahanati nyingi)
  • Umisheni na Uinjilisti
  • Upangaji na Maendeleo
  • Hudumu ya Jamii na Kazi ya Akinamama

Dayosisi

  • Dodoma
  • Iringa
  • Kati
  • Kaskazini
  • Kaskazini-Kati
  • Kaskazini-Mashariki[4]
  • Kaskazini-Magharibi[5]
  • Karagwe
  • Konde
  • Kusini
  • Kusini-Kati
  • Kusini-Magharibi
  • Kusini-Mashariki
  • Kusini-Mashariki kwa Ziwa Viktoria
  • Mashariki ya Ziwa Viktoria
  • Mashariki na Pwani
  • Mara
  • Mbulu
  • Meru
  • Morogoro
  • Pare
  • Ruvuma
  • Ulanga Kilombero
  • Ziwa Tanganyika

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads