Kachori

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Kachori ni vitafunio vya kukaanga sana, vinavyotokana na viazi mbatata ambavyo vimechemshwa na kupondwapondwa, kisha vimetiwa viungo mbalimbali, kama chumvi, ndimu na pilipili; hatimaye vikakaangwa kwa mafuta.

Asili yake ni Bara Hindi, na hujulikana katika maeneo na diaspora ya India na maeneo mengine ya Asia Kusini.

Kachori zilikuwa maarufu katika Indore ya zamani, hata kabla ya samosa kupata umaarufu baada ya kugawanywa kwa India. [1]

Banarasidas, mwandishi wa wasifu Ardhakathanaka, ametaja kununua kachori huko Indore mnamo 1613. [2] Kwa miezi saba, alinunua kachori kila siku, na alikuwa na deni la rupia ishirini. [3]

Inasemekana kachori imeanzia Uttar Pradesh, India.

Remove ads

Picha

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads