Kantarusi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kantarusi
Remove ads

Kantarusi (pia Kantori[1], Centaurus kwa Kilatini na Kiingereza) ni jina la kundinyota kwenye angakusi ya Dunia yetu.

Thumb
Centaurus Constellation chart
Thumb
Kentaurus - Kantarusi wa mitholojia ya Ugiriki

Lipo jirani na Salibu (en:Crux) likiwa na nyota mashuhuri ya Rijili Kantori (en:Alpha Centauri) iliyo nyota jirani na Jua letu kuliko zote.

Jina

Jina la Kantarusi lilijulikana tangu kale kwa mabaharia Waswahili waliotumia nyota hizo kutafuta njia yao baharini wakati wa usiku.

Asili ya jina ni Kigiriki Κένταυρος Kentauros, au Kilatini chake kiliichoingia katika lugha za Ulaya kama en:Centaurus. Kiarabu kilipokea jina la Kigiriki kwa umbo la قنطورس qanṭawrus na kutoka hapo liliingia katika Kiswahili.

Kantarusi - Kentaurus ni kiumbe katika mitholojia ya Ugiriki ya Kale kinachounganisha mwili wa binadamu na farasi.

Remove ads

Nyota

Kantarusi ni kundinyota kubwa lililo na mbili za nyota angavu sana kwenye anga[2]. Nyota mashuhuri zaidi ni Rijili Kantori inayojulikana pia kwa jina la Bayer Alfa Centauri maana hii ni nyota iliyo jirani zaidi nasi katika anga-nje ikiwa na umbali wa miakanuru 4.3. Pamoja na Hadar (Beta Cent) ambayo ni pia nyota angavu hizi mbili zinadokeza kwa Salibu (Crux). Rijili Kantori na pia Hadar ni nyota maradufu.


Maelezo zaidi B, F ...

Katika eneo la Kantarusi kuna fungunyota kadhaa; ω Centauri inaonekana kwa macho matupu kuwa doa dogo na kwa darubini tu nyota kadhaa ndani yake zinatambuliwa[3].

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads