Kariakoo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kariakoo
Remove ads

Kariakoo ni kata ya wilaya ya Ilala katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 11106.

Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...
Thumb
Soko la Kariakoo

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 10,246 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,780 waishio humo.[2]

Kariakoo inajulikana kutokana na soko kubwa.

Remove ads

Asili ya jina

Jina la eneo hili ni la kihistoria: linatokana na neno la Kiingereza "carrier corps", yaani kikosi cha wapagazi waliobeba mizigo ya jeshi wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Pande zote vitani walitumia malakhi ya wapagazi waliokodishwa au kulazimishwa kufanya huduma hii.

Baada ya vita wapagazi kadhaa walipewa maeneo ya kujenga nyumba kwenye miji mbalimbali na hivyo majina kama "Kariakoo" au "Kariokor" (Nairobi) yanapatikana katika miji mbalimbali ya Afrika ya Mashariki.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads