Mkoa wa Dar es Salaam

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoa wa Dar es Salaam
Remove ads

Mkoa wa Dar es Salaam ni mojawapo ya mikoa ya Tanzania ulioko katika pwani ya mashariki mwa Tanzania. Unapakana na Mkoa wa Pwani upande wa magharibi, kaskazini, na kusini, huku upande wa mashariki ukipakana na Bahari ya Hindi. Ni mkoa mdogo zaidi kwa ukubwa wa eneo (km² 1,393 pamoja na visiwa vidogo 8), lakini una idadi kubwa zaidi ya wakazi nchini, ukiwa na watu takriban 5,383,728 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022,[1] tena ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani. Ingawa Dodoma ni mji mkuu wa kisiasa, Dar es Salaam inabaki kuwa makao makuu ya taasisi nyingi za serikali, mashirika ya kimataifa, na sekta binafsi. Pia ni kitovu cha shughuli za biashara, uchumi, na usafirishaji nchini, na inahudumia pia nchi za jirani kupitia bandari ya Dar es Salaam.Mkoa huu una wilaya tano: Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, na Kigamboni.

Thumb
Mahali pa Mkoa wa Dar es Salaam katika Tanzania.
Thumb
Dar es Salaam miaka ya 1930.
Thumb
Uwanja wa Taifa
Thumb
Machweo jijini
Thumb
Ghorofa ndefu kuliko zote za Afrika Mashariki.
Thumb
Makao makuu ya Benki kuu ya Tanzania.
Thumb
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Thumb
Shamba la Mungu.

Wakazi asili wa eneo la mkoa ni Wazaramo ingawa kwa sasa kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji, kuna makabila yote ya Tanzania, mbali ya wageni wengi kutoka nchi mbalimbali.

Remove ads

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

  • Ilala : mbunge ni Mussa Azzan Zungu (CCM)
  • Kawe : mbunge ni Joseph Gwajima (CCM)
  • Kibamba : mbunge ni (CCM)
  • Kigamboni : mbunge ni Faustine Ndugulile (CCM)
  • Kinondoni : mbunge ni Abbas Tarimba (CCM)
  • Mbagala : mbunge ni Issa Ally Mangungu (CCM)
  • Segerea : mbunge ni Bonna Mosse Kaluwa (CCM)
  • Temeke : mbunge ni Abdallah Mtolea (CCM)
  • Ubungo : mbunge ni Kitila Mkumbo (CCM)
  • Ukonga : mbunge ni Jerry Silaa (CCM)
Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads