Katibu Mkuu wa UM

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mtendaji mkuu wa UM na mwenyekiti wa Ofisi Kuu ya UM ambayo ni kati ya vitengo muhimu vya Umoja wa Mataifa.

Uteuzi wa Katibu Mkuu

Katibu Mkuu huchaguliwa na Mkutano Mkuu wa UM kwa muda wa miaka mitano. Jina linapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu na Baraza la Usalama la UM. Kwa hiyo uteuzi wa Katibu Mkuu uko mkononi mwa Baraza la Usalama na kila taifa mjumbe wa kudumu linaweza kuzuia jina fulani lisipelekwa kwa njia ya Veto yake. Lakini Baraza la Usalama linapaswa kumteua mtu atakayepata kura za kutosha katika Mkutano Mkuu.

Hakuna sheria juu ya muda wa kazi yake lakini hadi sasa hakuna Katibu Mkuu aliyehudumia UM zaidi ya vipindi viwili au miaka 10. Kuna kawaida ya kwamba nafasi ya Katibu Mkuu inapita kwenye mabara yote ingawa hiyo si sheria.

Mshahara wa Katibu Mkuu ni dolar za Marekani 176,877 kwa mwaka. (2006).

Remove ads

Orodha ya Makatibu Wakuu

Maelezo zaidi #, Picha ...
Remove ads

Makamu wa Katibu Mkuu

Mkutano Mkuu uliamua 1997 kuanzisha cheo kipya cha makamu wa Katibu Mkuu.

Tangu 7 Januari 2007 Asha-Rose Migiro kutoka Tanzania amepewa nafasi hii. Alimfuata Mark Malloch Brown.


Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads