Khoikhoi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Khoikhoi
Remove ads

Khoikhoi (au Khoekhoe[1]; kwa lugha yao maana ni "watu watu", "watu halisi"[2] [3]) ni wakazi asili wa Kusini mwa Afrika pamoja na Wasan, ambao kwa jumla wanaitwa Khoisan.

Thumb
Mwanamume Khoikhoi.
Thumb
Wakhoikhoi wakijiandaa kuhama na mahema yao. Mchoro wa Samuel Daniell (1805).

Tofauti kati yao ni hasa utamaduni, kwa maana Wasan (kwa maana halisi "Wagunduzi").[4] wanaendelea kwa kiasi kikubwa kuishi kwa uwindaji, wakati Khoikhoi toka muda mrefu wanategemea ufugaji wa kuhamahama na kilimo[5].

Kadiri ya akiolojia walifikia eneo la Cape Town miaka 2,000 iliyopita wakitokea kaskazini (Botswana ya leo).

Kuanzia karne ya 3 BK walifikiwa na wavamizi wa Kibantu waliojitwalia maeneo mazuri zaidi.

Ingawa ni wazi kuwa uwepo wa Khoekhoen Kusini mwa Afrika unatangulia upanuzi wa Wabantu, kulingana na nadharia ya kisayansi inayotokana na ushahidi wa kilugha, haijulikani ni lini Wakhoekhoe walianza kukaa katika maeneo ambayo mawasiliano ya kwanza na Wazungu yalitokea (labda katika Umri wa Jiwe la kale).[4] Wakati huo, katika karne ya 17, Wakhoekhoe walitunza ng'ombe wengi wa aina ya Nguni katika mkoa wa Cape. Ufugaji wao wa kuhamahama uliachwa zaidi katika karne ya 19 hadi ya 20.[6]

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads