Kinahuatl
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kinahuatl (nāhuatl, mexìcatlàtōlli) ni kati ya lugha asilia za Meksiko zilizopo tangu kabla ya kufika kwa Wahispania. Idadi ya wasemaji wa lahaja zake ni takriban milioni moja na laki saba.
Ilikuwa lugha ya Waazteki, Watolteki na wengine wa nyanda za juu za Meksiko. Tangu kufika kwa ukoloni lahaja mbalimbali zilijitokeza na sasa si wasemaji wote wanaoelewa wasemaji wote wengine.
Maneno ya Kinahuatl yalitaja mazao yaliyopelekwa kote duniani pamoja na majina yake. Kati ya maneno ya Kinahuatl yaliyosambaa duniani ni:
- (āhuacatl) avocado (parachichi)
- (cacahuatl) kakao
- (chīlli) chili (pilipili kali)
- (xōchiyōcacahuatl) chokoleti
- tequila (pombe kali ya Kimeksiko)
- (tomātl) tomato (nyanya)
Majina ya nchi za Meksiko, Guatemala na Nikaragua yana asili za Kinahuatl vilevile.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kinahuatl kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads