Uhispania

nchi katika Ulaya Kusini-Magharibi From Wikipedia, the free encyclopedia

Uhispania
Remove ads

Uhispania (Kihispania: España; Kiingereza: Spain) kwa rasmi Ufalme wa Hispania, ni nchi iliyoko Kusini-magharibi mwa Ulaya ikiwa na maeneo katika Kaskazini mwa Afrika. Ikiwa na sehemu ya kusini kabisa ya bara la Ulaya, ni nchi kubwa zaidi katika Ulaya ya Kusini na ya nne kwa idadi ya watu miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Inashika maeneo makubwa ya Rasi ya Iberia, na eneo lake pia linajumuisha Visiwa vya Canary, vilivyoko Mashariki mwa Bahari ya Atlantiki, Visiwa vya Balearic, vilivyoko Magharibi mwa Bahari ya Mediterranean, na miji ya kiutawala ya Ceuta na Melilla, katika Afrika.

Ukweli wa haraka Uhispania Reino de España (es), Mji mkuu na mkubwa ...
Remove ads

Kuna pwani ndefu ya Bahari ya Mediteranea na pia ya Atlantiki.

Uhispania bara ni sehemu kubwa ya rasi ya Iberia. Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea na Visiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja na miji ya Afrika ya Kaskazini Ceuta na Melilla ni sehemu za Uhispania.

Mji mkuu ni Madrid ambayo ni pia mji mkubwa wa nchi.

Eneo la nchi ni km² 505,990 nalo lina wakazi 47,450,795 (sensa ya mwaka 2020).

Mfalme Felipe VI amevaa taji mwaka 2014, akishika nafasi ya baba yake Juan Carlos I, anayeheshimiwa sana kwa sababu aliongoza taifa katika mabadiliko ya kutoka udikteta wa jenerali Francisco Franco kuelekea demokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuia mapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana.

Muundo wa serikali ni Ufalme wa Kikatiba, hivyo kisheria madaraka ya mfalme ni madogo.

Utawala umo mikononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge linaloitwa "Las Cortes likichaguliwa kwa kura za kidemokrasia.

Remove ads

Historia

Historia ya awali

Wakazi wa kwanza waliojulikana kwa jina kuwa waliishi Uhispania walikuwa Wakelti.

Wafoinike

Katika karne za KK Wafoinike walianzisha miji kwenye pwani na kuchimba madini hasa shaba na fedha.

Waroma

Waroma wa Kale walivamia na kutawala Uhispania kwa karne kadhaa wakileta lugha yao ya Kilatini kilichopata kuwa msingi wa lugha za kisasa za Uhispania. Kibaski pekee si lugha ya Kirumi.

Katika karne ya 5 makabila ya Kigermanik walivamia Dola la Roma pamoja na Uhispania. Kati yao Wavandali na Wavisigothi walitawala sehemu kubwa ya Uhispania.

Waarabu

Tangu mwaka 711 jeshi la Waarabu Waislamu liliingia kutoka Afrika ya Kaskazini na kutwaa sehemu kubwa ya Uhispania hadi karibu milima ya Pirenei, lakini watawala wa maeneo kadhaa katika kaskazini walijihami na kufaulu kudumisha uhuru wao.

Waarabu walileta fani nyingi za maendeleo nchini.

Katika kipindi cha vita cha karne nyingi Wakristo wa Kaskazini walifaulu polepole kuwarudisha nyuma Waarabu hadi kusini kwa nchi.

Hatimaye mwaka 1492 mfalme Boabdil wa Granada, mji wa mwisho wa Waarabu, alishindwa na mfalme Ferdinand II wa Aragon na malkia Isabella wa Kastilia.

Makoloni ya Amerika

Wiki chache kabla ya kushinda huko Granada wafalme wa Uhispania walimkubalia nahodha Kristoforo Kolumbus kutafuta njia ya kufika Bara Hindi kupitia magharibi. Badala ya kufika India Kolumbus alifika kwenye visiwa vya Amerika ya Kati.

Huo ulikuwa mwanzo wa upanuzi wa Uhispania katika "Dunia Mpya" ya Amerika. Wahispania walijenga dola kubwa la kikoloni na kutwaa karibu Amerika ya Kusini yote pamoja na Amerika ya Kati na Mexiko hadi sehemu za kusini za Marekani ya leo.

Katika miaka mia tatu iliyofuata Uhispania ilitajirika sana kutokana na maliasili ya Amerika.

Vita vya Marekani dhidi ya Uhispania

Vita hivyo vilitokea mwaka 1898. Vilianza kwa shambulizi la Marekani tarehe 25 Aprili dhidi ya Puerto Rico vilivyokuwa koloni la Uhispania na kuishia tarehe 12 Agosti 1898, jeshi la Uhispania huko Manila (Ufilipino) liliposalimu amri.

Vita hivyo vilikuwa mwanzo wa Marekani kufuata siasa ya nje ya upanuzi hata katika maeneo ya mbali. Kabla ya vita hivyo Marekani ilishughulika kupanua eneo lake kwenye bara la Amerika ya Kaskazini dhidi ya wakazi asilia na dhidi ya Mexiko.

Marekani ilitumia nafasi ya ghasia ya wenyeji wa Kuba dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uhispania.

Baada ya mlipuko kwenye manowari ya Marekani USS Maine katika bandari ya Havana, Marekani ilitangaza vita dhidi ya Uhispania ingawa sababu ya mlipuko haijajulikana hadi leo ilikuwa nini.

Uhispania haikuweza kushindana na manowari na silaha za Marekani zilizokuwa zimeendelea kiteknolojia.

Pia Marekani ilikuwa karibu na mahali pa vita na Uhispania ilishindwa kuongeza wanajeshi na silaha.

Hivyo Marekani ilitwaa makoloni ya Uhispania ya Puerto Rico, Kuba na Ufilipino.

Remove ads

Jiografia

Thumb
Ramani ya Uhispania.

Majimbo ya kujitawala

Thumb
Ramani ya majimbo 17 ya Uhispania.
Maelezo zaidi Bendera, Jimbo la kujitawala ...

R.A: Regionally appointed; D.E: Directly elected.

Miji ya kujitawala

Maelezo zaidi Bendera, Mji wa kujitawala ...

Marundiko ya miji mikubwa

Remove ads

Watu

Wakazi walio wengi (84.8%) ni Wahispania asili, lakini uhamiaji mkubwa wa miaka ya mwisho umeleta watu wengi hasa kutoka Amerika ya Kilatini, Afrika Kaskazini, Ulaya Mashariki n.k.

Lugha rasmi ni Kihispania inayozungumzwa nyumbani na 74% za watu lakini majimbo 17 yamepewa mamlaka ya kujitawala katika mambo mbalimbali pamoja na sera za kiutamaduni, hivyo lugha za Kikatalunya (17%), Kigalicia (7%), Kibaski (2%) na Kioccitan zimekuwa lugha rasmi za kijimbo pamoja na Kihispania.

Wahispania walio wengi (61%) ni waamini wa Kanisa Katoliki. 34% hawana dini yoyote.

Remove ads

Picha

Tazama pia

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads