Kinara cha taa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kinara (kwa Kiing. candelabra) ni kifaa cha kusimamishia mishumaa ndani yake ili itumike kama taa [1]. Huwa na idadi ya matawi ambayo kila moja linabeba mshumaa mmoja. Siku hizi kuna pia vinara vyenye balbu ilhali umbo la kinara huchaguliwa kama pambo la nyumba.


Katika historia kulikuwa na vinara ambavyo mafuta badala ya mishumaa yanawaka. Kinara cha aina hiyo ni menorah ya Kiyahudi yenye matawi 7.
Vinara hujulikana kutoka tamaduni mbalimbali ya kale[2].
Jina la Kiswahili limetokana na mnara likiwa na maana ya "mnara mdogo".
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads