Mshumaa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mshumaa
Remove ads

Mshumaa (kwa Kiingereza candle, kutokana na Kilatini candēla, neno ambalo linategemea kitenzi candēre, kuangaza.[1]) ni kifaa cha kuletea mwanga gizani kinachotengenezwa kwa nta au kemikali fulani.

Thumb
Mshumaa ukinunuliwa dukani huko Zambia.
Thumb
Mvulana na mshumaa, mchoro wa Michel Gobin.
Thumb
Mkusanyo wa mishumaa ya kikemikali ya kisasa.

Unaweza kuwashwa pia kwa sababu ya kuleta harufu au joto, au hata kwa kupima muda[2].

Ili kushika mshumaa, tangu zamani vilitengenezwa vinara vya thamani tofautitofauti na hata vilivyopambwa kwa sanaa.[3]

Mshumaa unawashwa kwa kiberiti, halafu unaendelea wenyewe huku ukiyeyuka taratibu.[4]

Remove ads

Historia

Mishumaa ya zamani zaidi kati ya ile iliyopo hadi leo ilitengenezwa huko China miaka 200 KK hivi, na ilifanywa kwa mafuta ya nyangumi.[5]

Thumb
Mshumaa ukiwaka katika monasteri ya Visoki Dečani.

Kabla ya kuvumbua namna ya kutengeneza umeme, mishumaa na taa za mafuta ndivyo vilivyotumika kuleta mwanga, kama ilivyo bado umeme huo usipopatikana.

Lakini katika nchi zilizoendelea, mishumaa inatumika bado kwa mapambo tu, hasa mahali pa ibada au kuhusiana nayo. [6] Muhimu kuliko yote ni mshumaa wa Pasaka.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads