Kipengele
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kipengele (pia: Kipengere) ni kata ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59314.
Kata iko mguuni pa milima ya Kipengere.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 9,051 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,273 [2] walioishi humo.
Watu hao hujihusisha na kilimo cha viazi, maharage, tetere, mbogamboga, mahindi; kwa utamaduni wao wanakula pamoja kwenye sahani moja ugali wanaousonga kwenye chungu.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads