Mkoa wa Njombe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mkoa wa Njombe ni mmojawapo kati ya mikoa mipya nchini Tanzania ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012[1]. Umepakana na mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya na Iringa, mbali ya Ziwa Nyasa. Mkoa una eneo la km2 21,347 na wakazi 889,946 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [2], ukishika nafasi ya mwisho kati ya mikoa ya Tanzania Bara. Makao makuu yako Njombe mjini.

Remove ads
Historia na demografia
Mkoa wa Njombe ulianzishwa mwaka 2012 kutokana na wilaya ya Njombe, Makambako, Makete na Ludewa. Kutokana na hadhi mpya, wilaya ya Njombe imegawanyika kati ya ile ya mjini na ile ya vijijini. Pia, mwezi wa Machi 2012, imeanzishwa wilaya ya Wanging'ombe. Mwaka 2012 katika eneo hilo kulikuwa na wakazi 702,097 [3] katika wilaya sita zifuatazo: Njombe Mjini (wakazi 130,233), Njombe Vijijini (wakazi 85,747), Makambako (wakazi 93,827), Makete (wakazi 97,266), Ludewa (wakazi 133,218), Wanging'ombe (wakazi 161,816).
Mwaka 20222 mchanganuo katika wilaya zake sita ni kwama ifuatavyo: Njombe Mjini (wakazi 182,127), Njombe Vijijini (wakazi 109,311), Makambako (wakazi 146,481), Makete (wakazi 109,160), Ludewa (wakazi 151,361), Wanging'ombe (wakazi 191,506).
Makabila makubwa ya wenyeji mkoani Njombe ni Wabena, Wakinga na Wapangwa, na uwiano wao ni 37:11:3.
Kabila la Wabena liko wilaya ya Njombe na eneo la Malangali likiwa linapakana na wilaya ya Ulanga na wilaya ya Mlimba (Mkoa wa Morogoro), Wakinga wako wilaya ya Makete na Wapangwa wako katika wilaya ya Ludewa.
Yapo pia makabila madogo kama vile Wawanji, Wakisi, Wamanda, Wamagoma n.k. ambao kwa ujumla wao wanachukua asilimia 6 iliyosalia ya watu mkoani.
Karibu wakazi wote wa mkoa ni Wakristo, hasa Walutheri na Wakatoliki.
Remove ads
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Njombe Kaskazini : mbunge ni Joram Hongoli (CCM)
- Njombe Kusini : mbunge ni Edward Mwalongo (CCM)
- Makambako : mbunge ni Deo Kasenyenda Sanga (CCM)
- Wanging'ombe : mbunge ni Gerson Hosea Lwenge (CCM)
- Makete : mbunge ni Dk. Norman Adamson Sigalla (CCM)
- Ludewa : mbunge ni Ndugu. Joseph Zacharius Kamonga (CCM)
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads