Kipolandi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kipolandi
Remove ads

Kipolandi (kwa lugha asilia: język polski) ni lugha ya Kislavoni cha Magharibi inayozungumzwa hasa nchini Polandi. Ni lugha rasmi ya taifa hilo na inazungumzwa na takribani watu milioni 40 kama lugha ya kwanza, pamoja na zaidi ya milioni 2.1 wanaoitumia kama lugha ya pili, hususan miongoni mwa jamii za Kihamiaji barani Ulaya, Amerika Kaskazini, na Australia. Kipolandi ni mojawapo ya lugha kubwa zaidi katika familia ya lugha za Kislaviki, na hutumia alfabeti ya Kilatini yenye herufi 32, zenye alama za matamshi za kipekee kama vile ą, ć, ę, ł, ń, ó, ś, ź, ż.

Ukweli wa haraka Kipolandi język polski (pl), Lugha ...

Kipolandi kina historia ndefu na tajiri, kimeathiriwa na lugha nyingine za Ulaya kama vile Kijerumani, Kilatin, na Kirusi, hasa katika nyanja za fasihi, siasa na elimu. Fasihi ya Kipolandi imechangia kwa kiasi kikubwa utamaduni wa Ulaya Mashariki, na waandishi wa Kipolandi kama Adam Mickiewicz na Wisława Szymborska wametambuliwa kimataifa. Leo hii, Kipolandi pia hutumika katika taasisi za Ulaya kama mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Ulaya, na ni lugha muhimu katika biashara, elimu ya juu, na diplomasia katika kanda ya Ulaya ya Kati.

Remove ads

Herufi

Kuna takriban herufi 9 za Kipolandi ambazo katika Kiingereza hakuna. Zinaonekana kuwa kama Kiingereza, lakini zenyewe zinaviji alama kwa juu au kwa chini.

Katika herufi ndogo, herufi tisa ni: ą ć ę ł ń ó ś ź ż

Katika herufi kubwa, herufi tisa ni: Ą Ć Ę Ł Ń Ó Ś Ź Ż

Kuna herufi 3 katika Kiingereza ambazo katika Kipolandi hazitumiki: q, v, x.

Kuna mchanganyiko wa herufi 7 katika kila herufi 2 ambazo zote zinaonekana kuwa kama sawa katika kusikika (ambazo sawa na "th" au "qu" katika Kiingereza). Ambazo zimejumlisha herufi kama vile "ch", "cz", "dz", "dź", "dż", "rz", "sz", "szcz".

Remove ads

Kusikika

Lafudhi

Lugha ya Kipolandi ina lafudhi nyingi sana, lakini ni chache mno kuliko lugha zingine za Ulaya. Kuna utofauti mdogo tu katika Kipolandi cha "kawaida", lakini kila mwongeaji anaweza kumwelewa mwenziwake, na wale ambao wao sio wazawa wa lugha hiii kawaida hawezi kujua tofauti zao katika kutamka.

Maneno kadhaa ya Kipolandi

ja - mimi
ty - wewe
on - yeye
my - sisi
oni - wao

co? - nini?
kto? - nani?
gdzie? - mahali gani?
dokąd? - wapi?
kiedy? - hini?
jak? - vipi?
dlaczego? - kwanini?
który? - ipi?

Namba:

moja - jeden
mbili - dwa
tatu - trzy
nne - cztery
tano - pięć
sita - sześć
saba - siedem
nane - osiem
tisa - dziewięć
kumi - dziesięć
kumi na moja - jedenaście
kumi na mbili - dwanaście
ishirini - dwadzieścia
ishirini na moja - dwadzieścia jeden
thelathini - trzydzieści
arobaini - czterdzieści
hamsini - pięćdziesiąt
mia moja - sto
elfu moja - tysiąc

Remove ads

Viungo vya nje

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads