Kiseyeye

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Kiseyeye (pia: hijabu; kwa Kiingereza scurvy) ni ugonjwa unaosababishwa na uhaba wa vitamini C mwilini. Dalili zake ni pamoja na kutokea kwa madoa kwenye ngozi. Meno yanaanza kuchezacheza na kupotea. Watu wanaweza kutokwa na damu mdomoni na puani. Viungo vya mwili huuma. Mgonjwa atakuwa dhaifu.

Zamani kiseyeye kilikuwa ugonjwa hasa wa mabaharia waliokaa muda mrefu kwenye maji bila kula matunda au chanzo kingine cha vitamini C. Kabla ya kugundua kwamba akiba ya limau ni dawa njema mabaharia wengi walikufa kutokana na kiseyeye[1].

Remove ads

Picha za dalili za kiseyeye

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads