Kitabu cha Yuditi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kitabu cha Yudith ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Biblia ya Kikristo.

Kimo katika Septuaginta na katika Agano la Kale la Kanisa Katoliki, la Waorthodoksi wengi na la baadhi ya Waprotestanti, lakini si katika Tanakh ya Uyahudi wala katika Biblia ya Waprotestanti.
Habari iliyomo
Hadithi hiyo, iliyoandikwa katika karne ya 1 KK inahusu wakati wa mfalme Nebukadreza II, na vita vyake dhidi ya Israeli (karne ya 6 KK).
Kinyume cha matarajio, Yudith, ambaye jina lake linamaanisha mwanamke wa kabila la Yuda, aliweza kupata ushindi mkubwa dhidi ya maadui wa taifa la Israeli kwa imani na ushujaa wake.
Habari hiyo ya ajabu ilipata mwangwi kwa wingi katika sanaa mbalimbali.
Ufafanuzi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads