Kleofa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kleofa
Remove ads

Kleofa (kwa Kigiriki Κλεόπας, Kleopas[1][2][3][4][5]) alikuwa Mkristo wa karne ya 1, maarufu kwa kutokewa na Yesu Kristo mfufuka akiwa njiani kutoka Yerusalemu kwenda Emau pamoja na mwanafunzi mwingine[6] (Lk 24:13-32).

Thumb
Kleofa na mwenzake wakikutana na Yesu njiani kadiri ya mchoro wa Joseph von Führich, 1837.

Simulizi la Injili ya Luka

Ilikuwa siku ya tatu baada ya kifo cha Yesu, ambayo ndiyo ya ufufuko wake kadiri ya Agano Jipya. Ingawa hao wanafunzi wawili walikuwa wamesikia kwamba kaburi la Yesu lilionekana tupu, hawakupata moyo wa kubaki mjini zaidi.

Njiani walikuwa wakishirikishana huzuni yao kwa sababu Yesu alishindwa kurudisha ufalme wa Israeli. Ghafla mgeni akaongozana nao na kuulizia sababu ya huzuni yao. Baadaye aliwakaripia kwa kukosa imani akawafafanulia utabiri wa Agano la Kale kuhusu Masiya. Hapo mioyo yao ilikuwa kama inawaka wanapomsikiliza [7].

Walipofikia kijijini walimuomba abaki nao usiku, lakini walipoanza kula, mgeni huyo alimega mkate: ndipo walipomtambua kuwa Yesu.

Hapo mwenyewe alitoweka, nao wakarudi mjini kupasha habari kwa mitume wake, waliomuambia kwamba Yesu amemtokea pia Simoni Petro.

Habari hiyo inasimuliwa kifupi na nyongeza ya Injili ya Marko pia (16:12-13).

Remove ads

Taarifa za baadaye

Mara nyingine Kleofa huyo anasemekana ndiye yule anayetajwa na Injili ya Yohane (19:25).[8]

Mwanahistoria, askofu Eusebius wa Kaisarea, anaripoti maandishi ya Hegesippus, ambaye mwaka 180 hivi BK alisema kwamba miaka ya nyuma aliwahi kudodosa wajukuu wa Mtume Yuda akajibiwa kuwa Kleofa alikuwa ndugu wa Yosefu, mume wa Bikira Maria [9]

Tangu kale Kleofa anaheshimiwa kama mtakatifu: na Wakatoliki tarehe 25 Septemba[10], na Waorthodoksi tarehe 30 Oktoba[11], na Wakopti tarehe 10 Novemba.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads