Krisogoni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Krisogoni
Remove ads

Krisogoni (alifariki Aquileia, leo nchini Italia, 303 hivi) alikuwa mwanamume Mkristo wa Roma ya Kale ambaye aliuawa kwa sababu ya imani yake, inawezekana sana wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano. Labda alikuwa padri kama si askofu [1].

Thumb
Mt. Krisogoni akiwa amepanda farasi alivyochorwa na Michele Giambono (San Trovaso, Venice).

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Wa kwanza wanaadhimisha sikukuu yake tarehe 24 Novemba[2], wa pili tarehe 22 Desemba (pamoja na Anastasia wa Sirmio anayesemekana alikuwa mwanafunzi wake).

Martyrologium Hieronymianum ilimuorodheshwa katika tarehe mbili tofauti: 31 Mei na 24 Novemba[3]

Krisogoni ni kati ya watakatifu wanaotajwa katika Kanuni ya Kirumi na wenye kanisa la zamani mjini Roma.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads