Krispino wa Viterbo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Krispino wa Viterbo
Remove ads

Krispino wa Viterbo (Viterbo, 13 Novemba 1668Roma, 19 Mei 1750) alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini.

Thumb
Mt. Krispino.

Mtu asiye na elimu, alijiwekea lengo la kulingana na bradha Felix wa Cantalice, mtakatifu wa kwanza wa shirika lake.

Alipokuwa anaombaomba sadaka katika vijiji vya milimani alikuwa anawafundisha wakulima misingi ya imani ya Kikristo[1].

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius VII tarehe 7 Septemba 1806, akawa mtakatifu wa kwanza kutangazwa na Papa Yohane Paulo II (20 Juni 1982).

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads