Leudini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Leudini (kwa Kifaransa: Leudin au Bodon; pia: Leudinus, Leudovinus, Leudvinus, Leudvin, Leudin, Lendin, Bodo; 625 hivi - 11 Septemba 678 hivi[1]) alikuwa askofu wa 17[2] wa Toul, leo nchini Ufaransa[3].

Kwanza alioa na kupata mtoto wa kike, lakini baadaye alikubaliana na mke wake Otilia waende kuishi kimonaki kama dada yake Salaberga[4]. Mwisho akawa askofu kwa miaka si mingi, kama miwili.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Septemba[5][6].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads