Nyege
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nyege au ashiki ni uchu au hamu ya kujamiana ambayo hupatikana kwa wanaume na kwa wanawake. Neno hili la Kilatini hutumika hasa mtu alipo na kiwango kidogo cha nyege. Hapo ndipo utakaposikia kwamba fulani ana nyege kidogo ama mwanamume fulani amekosa nguvu za kiume. Hata hivyo, yafaa ijulikane kwamba kuna tofauti kati ya hamu ya ngono na nguvu za kiume. Mwanamume asiye na nguvu za kiume huenda akawa na kiasi cha nyege kinachofaa, lakini hawezi kujamiana na mwenziwe kwa njia inayofaa maana mwili wake hauitikii.
Remove ads
Nyege husababishwa na nini
Nyege huathiriwa na sababu tofauti kama vile za biolojia, saikolojia na za kijamii.
Nyege huathirika kibiolojia kwa maana homoni za mwili, kama vile tesistosteroni na dopamini, husababisha mtu awe na uchu wa ngono au akose.
Unapokuwa na shida za kisaikolojia kama vile huzuni, wasiwasi au jambo linalokusumbua kiakili, basi uchu wako wa ngono pia utakwenda chini.
Kijamii, huenda ikawa kwamba kazi unazozifanya ili kukidhi mahitaji ya kila siku zinakunyima wakati au hata uchu wa ngono.
Nyege huenda ikaathirika iwapo u mgonjwa maana hutakuwa na uchu au hata fikra za ngono.
Remove ads
Nyege na umri
Utafiti umeonyesha kwamba wanaume huwa na nyege ya kiwango cha juu wanapobalehe kati ya umri wa miaka kumi na tano hadi kumi na tisa. Kutoka hapo, nyege yao yaenda ikididimia maana homoni ya tesistosteroni pia yafifia. Hata hivyo inasemekana [1] kuna uwezekano mtu akawa na nyege hafifu akiwa na umri mdogo ikiwa homoni yake ya tesistosteroni imekwenda chini, jambo ambalo linaweza kusuluhishwa .
Kwa upande mwingine, wanawake hupata nyege ya kiwango cha juu zaidi wanapofikia umri wa miaka thelathini. Ijapokuwa wao huanza tamaa ya ngono wakibalehe, hamu yao huwa juu zaidi wakiwa wenye umri huo wa miaka thelathini.
Remove ads
Dawa za kutitimua nyege
Kwa wanaume walio na nyege iliyo chini, kuna dawa ambazo waweza wakapewa na madaktari. Madawa haya, yanayotengenezwa kwa kemikali, au mata oganiki ikiwemo bidhaa zinazotolewa kwa mimea, wanyama na pia wadudu kama Spanish Fly, huwasaidia kuongezea kiwango cha homoni ya tesistosteroni testogen.
Kuna vyakula pia vinavyoongeza nyege kama vile ndizi, tini na parachichi. Matunda hayo hujulikana kama mkuyati (kwa Kiingereza aphrodisiacs)[2]. Mimea mingine mikuyati ni kama vile Muyohimbi (Pausinystalia yohimbe) wa Afrika Magharibi, Mkombelo (Mondia whytei) kutoka sehemu tofauti za Afrika na Muashwagandha kutoka Uhindi (Withania somnifera).[3]
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads