Lorcán Ua Tuathail
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Lorcán Ua Tuathail (pia: Laurence O'Toole; Castledermot, 1128 – Eu, 14 Novemba 1180[1][2]) alikuwa askofu mkuu wa Dublin, Ireland [3], wakati kisiwa hicho kilipovamiwa na Wanormani.


Katikati ya matatizo makubwa ya kipindi hicho cha vurugu, alichangia sana urekebisho wa Kanisa la huko kwa kupigania kwa nguvu zote nidhamu [4] pamoja na kupatanisha wenyeji na wavamizi. Alifariki akiwa safarini kumuendea mfalme Henri II wa Uingereza[5].
Tarehe 11 Desemba 1225 alitangazwa na Papa Honorius III kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Novemba[6].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads