Madilu System

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Jean de Dieu Makiese (alifahamika zaidi kwa jina la kisanii Madilu System, 28 Mei 1952 - 11 Agosti 2007) alikuwa mtunzi na mwimbaji wa muziki wa soukous.

Ukweli wa haraka Jina la kuzaliwa, Pia anajulikana kama ...

Alizaliwa huko mjini Léopoldville, enzi hizo iliitwa Kongo ya Kibelgiji - ambayo leo hii inajulikana kama Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Alipata kuwa mwanachama wa bendi ya soukous maarufu kama TPOK Jazz ambayo ilitamba sana katika tasnia ya muziki wa Kikongo katika miaka ya 1960 hadi 1980.[1]

Remove ads

Kazi ya muziki

Akiwa bwana mdogo mnamo mwaka wa 1969, Madilu aliimba na "Orchestre Symba", "Orchestre Bambula", iliyokuwa ikiongozwa na Papa Noel, na vilevile aliimba na "Festival des Maquisards", iliyokuwa ikiongozwa na Sam Mangwana. Madilu baadaye akaanzisha bendi yake mwenyewe iliyokuwa inajulikana kama "Orchestre Bakuba Mayopi".

Hata hivyo, haikutamba kivile hadi hapo alipoungana na Franco, hapo ndipo alipoanza kuwa mwimbaji maarufu sasa wa Kikongo na kuwa nyota maarufu wa Kimataifa. Franco ndiye aliyempachika jina la Madilu System, jina ambalo baadaye lilidumu. Kibao kikali cha kwanza cha Madilu akiwa na TPOK Jazz kilikuwa “Mamou (Tu Vois),” ambacho kilitamba sana mnamo mwaka wa 1984. Hilo lilipelekea Madilu kumiliki tungo yake mwenyewe katika bendi, “Pesa Position.” Baadaye ikaja “Mario” na “Reponse de Mario” mnamo mwaka wa 1985 na huenda hii ilikuwa moja kati ya kazi bab-kubwa zilizofanywa pamoja kati ya Franco-Madilu, “La Vie des Hommes” mnamo 1986.

Kufuatia kifo cha Franco, TPOK Jazz ilisimama kutengeneza muziki kwa muda wa mwaka mmoja. Kisha kundi likarudi tena lakini safari hii na Madilu akiwa kama kiongozi mkuu. Miaka iliyofuata, alikuwa kiungo kikuu cha bendi katika kuunganisha upya bendi, kote jukwaani na studio. Madilu baadaye akaenda kuanzisha bendi yake binafsi yenye mafanikio makubwa. Baadaye akahamishia makazi yake huko mjini Paris, Ufaransa na baadaye Geneva, Uswizi, huku akidumisha kikosi kikubwa cha mashabiki zake wa nyumbani huko mjini Kinshasa.

Mwanzoni mwa mwezi wa Agosti 2007, Madilu alisafiri hadi mjini Kinshasa kwenda kupiga video kwa ajili ya nyimbo zake mpya. Alianguka Ijumaa ya tarehe 10 Agosti, 2007. Alipelekwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Kinshasa, ambapo alifia asubuhi yake iliyofuata, Jumamosi ya tarehe 11 Agosti, 2007.[2]

Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads