Mahé
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mahé ni kisiwa kikubwa cha funguvisiwa la Shelisheli. Urefu wake ni km 28 na upana wake km. 8. Eneo lake ni km² 154,7.
Mahe ina wakazi 72,000 ambao ni sawa na asilimia 90 za wakazi wote wa Shelisheli.
Mji mkubwa ni Victoria ambao ni pia mji mkuu wa taifa la Shelisheli.
Biashara kuu ya Mahe ni utalii. Karibu watalii wote wanaotembelea visiwa wanapita kwenye uwanja wa ndege wa Victoria.

Sehemu kubwa za Mahe zimefunikwa na misitu minene. Mlima mkubwa ni Morne Seychellois wenye kimo cha mita 905 juu ya UB.
Kisiwa kilitembelewa na Waingereza mnmo mwaka 1609 na wakati ule haukuwa na wakazi. Wafaransa waliunda makazi ya kwanza ya kudumu mnamo 1742 wakaanzisha mashamba na kuchukua wafungwa kama watumwa waliolima mashamba hayo. Mwaka 1814 Mahe pamoja na funguvisiwa vilitwaliwa na Uingereza na kuwa koloni lake hadi uhuru wa nchi mwaka 1976.
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mahé kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads